• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Okello aelekea Paradou, uhamisho wa Kizza wakumbwa na vikwazo

    (GMT+08:00) 2020-01-16 17:22:36

    Allan Okello anaweza kujiunga na timu ya Paradou FC mapema mwishoni mwa wiki hii kama kila kitu kikienda sawa. Mchezaji huyo mwenye kipaji kutokea timu ya KCCA ya Uganda anaweza kuondoka kesho kuelekea Algeria kwa ajili ya kupima afya kabla ya kukamilisha uhamisho huo. Wakati Okello akiwa njiani kuelekea Algeria, mchezaji mwenzake Mustaffa Kizza amerejea nyumbani. Kizza aliondoka Uganda Jumanne kwenda Morocco kwa ajili ya vipimo vya afya, lakini klabu ya Agadir ya nchini Morocco imeiarifu KCCA kusitisha uhamisho wa Kizza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako