• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Misri, Ethiopia na Sudani kuendelea kujadili ujazaji maji kwenye bwawa

  (GMT+08:00) 2020-01-16 19:35:33

  Mawaziri kutoka Misri, Ethiopia na Sudani wamekubaliana kukutana tena mjini Washington baadaye mwezi huu kukamilisha makubaliano ya bwawa kubwa la umeme kwenye mto wa Blue Nile ambalo lilizua mzozo wa kidiplomasia kati ya Cairo na Addis Ababa.

  Mawaziri hao walikutana huko Washington wiki hii na kukubaliana kujaza maji bwawa hilo la gharama ya dola bilioni 4 katika awamu kadhaa wakati wa mvua.

  Mpango wa kwanza wa kujaza maji kwenye bwawa hilo unatarajiwa kuanza mwezi Julaina kuanza uzalishaji wa umeme.

  Taarifa ya pamoja ya mawaziri hao inasema watafanya mazungumzo ya kiufundi na kisheria mbele ya mkutano wao wa Januari 28-29 huko Washington, ambapo wanapanga kukamilisha makubaliano hayo.

  Misri imekuwa na hofu kwamba bwawa hilo, litazuia usambazaji wa maji kwenye mto Nile ambayo yanategemewa na zaidi ya watu milioni 100.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako