• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya China na Russia hautathirika na mchakato wa siasa ya ndani ya nchi hizo

    (GMT+08:00) 2020-01-16 20:01:45

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Geng Shuang amesema, uhusiano wa kiwenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia hautaathirika na mabadiliko ya kimataifa na mchakato wa kisiasa wa ndani ya nchi hizo.

    Bw. Geng amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari hapa Beijing. Amesema kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Russia Bw. Dmitry Medvedev na serikali yake ni siasa za ndani ya nchi hiyo, na China inaheshimu hatua hiyo ikiwa nchi jirani na rafiki.

    Bw. Geng ameongeza kuwa chini ya uongozi wa kimkakati wa Rais Xi Jinping wa China na Rais Vladimir Putin wa Russia, uhusiano wa kiwenzi wa ushirikiano wa kimkakati umeingia katika zama mpya, na kuwa na utulivu, na China ina imani katika kuimarisha na kuendeleza uhusiano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako