• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Zimbabwe zaahidi kuimarisha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:23:23

    Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Guo Shaochun amesema China itaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na Zimbabwe, wakati nchi hizo mbili zinaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yao.

    Akizungumza kwenye tafrija iliyofanyika mjini Harare kukaribisha msimu wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Balozi Guo ameeleza imani yake kuwa uhusiano wa kibalozi uliodumu kwa miongo minne kati ya nchi hizo mbili, utaweka msingi wa mustakbali mzuri katika siku zijazo.

    Naye mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa ya Zimbabwe Bw. Lovemore Mazemo ambaye pia alihudhuria tafrija hiyo, amewashukuru wachina kutokana na uungaji mkono wao kwa mahitaji ya kimaendeleo ya Zimbabwe.

    Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kuinua kiwango cha kuaminiana kisiasa na kuimarisha ushirikiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako