• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatafakari ushirikiano wa huduma za kizahanati za madaktari bingwa nchini Namibia

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:23:41

    Serikali ya China inatafuta kupanua ushirikiano kwenye sekta ya afya nchini Namibia na kuanzisha ushirikiano katika huduma za kizahanati za madaktari bingwa kama upasuaji wa ubongo katika siku zijazo.

    Balozi wa China nchini Namibia Bw. Zhang Yiming amesema hayo jana alipoiaga timu ya 12 ya madaktari wa China ambao walianza kutumiwa nchini Namibia tangu mwaka 2018.

    Balozi Zhang amesema China inafikiria kuanzisha hospitali zenye ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na pia inatarajia kutoa fursa nyingi zaidi za mafunzo na udhamini kwa madaktari bingwa wa Namibia.

    Imefahamika kuwa timu ya 12 ya madaktari wa China nchini Namibia ilitoa huduma za Tiba ya Jadi ya Kichina kwa wagonjwa zaidi ya 20,000 katika kipindi chao cha mwaka mmoja na nusu kwenye hospitali ya taifa ya Katutura na vituo vingine vya afya nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako