• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za kusini mwa Afrika zakabiliwa na njaa kutokana na mabadiliko ya tabianchi

     

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:46:05
    Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetoa wito wa fedha zaidi kwa ajili ya juhudi zake za kupambana na njaa katika nchi za kusini mwa Afrika ambazo watu wengi wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya ya kiuchumi. Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo inasema, watu milioni 45 kati ya watu milioni 345 wa kanda hiyo ambao wengi ni wanawake na watoto, wanakumbwa vibaya na njaa kufuatia ukame wa mara kwa mara, mafuriko na hali mbaya ya kiuchumi. Taarifa hiyo inasema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua ili kuwaokoa. Lakini hadi sasa WFP imepata dola milioni 205 tu za kimarekani, huku ikihitaji dola milioni 489.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako