• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana na kuporomoka kwa jengo Uganda yaongezeka na kufikia watano 

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:46:51

    Idadi ya vifo kutokana na kuporomoka kwa jengo linalojengwa katika mkoa wa mashariki wa Jinja nchini Uganda imeongezeka na kufikia watano, na wengine 12 wameokolewa. Msemaji wa polisi eneo la Kiira Bibi Diana Nandaula amesema waokoaji wanafanya utafutaji kwenye kifusi kuona kama kuna watu wamekwama. Ajali za kuanguka kwa majengo yanayojengwa zinatokea mara kwa mara nchini Uganda, haswa kutokana na hali duni ya ujenzi. Tarehe 9 mwezi huu, karibu wafanyakazi sita walikufa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya jengo lililokuwa linajengwa kuporomoka mjini Kampala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako