• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: UEFA yabadili mfumo wa kikosi cha mwaka kwa kumtoa Ng'olo Kante na kumuweka Cristiano Ronaldo

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:51:00

    Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limebadili mfumo wa kikosi cha mwaka kilichopigiwa kura na mashabiki kwa kumtoa Ng'olo Kante na kumuweka Cristiano Ronaldo. Kikosi hicho kilichopigiwa kura na mashabiki dunia nzima kilitangazwa Jumatano, Januari 15, 2020 kikiwa na mfumo wa 4-2-4, ambapo wachezaji waliotajwa katika kikosi hicho ni Golikipa: Alisson, Walinzi: Trent Alexander-Arnold, Matthijs De Ligt, Virgil Van Dijk na Andy Robertson, Viungo: Frenkie De Jong na Kevin De Bruyne pamoja na Washambuliaji: Lionel Messi, Robert Lewandowski, Cristiano Ronaldo na Sadio Mane. Inaelezwa kuwa Ronaldo alipata kura chache dhidi ya washambuliaji wenzake, Messi, Lewandowski na Mane na wakuu wa shirikisho hilo hawakuridhishwa na Ronaldo kuachwa kwake, hivyo wakaamua kufanya mabadiliko hayo na kupelekea sintofahamu kubwa. Inadaiwa kuwa kikosi hicho kilikuwa tayari kutangazwa tangu wiki iliyopita lakini suala la Ronaldo ndilo lililopelekea kucheleweshwa kwa taarifa hiyo kutangazwa

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako