• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Venus Williams apangiwa na kinda Coco Gauff kwenye Grand Slam

    (GMT+08:00) 2020-01-17 09:51:53

    Mmarekani Coco Gauff atakabiliana tena na Venus Williams katika raundi ya kwanza ya Grand Slam baada ya wawili hao kuwekwa pamoja kwenye michuano ya wazi ya Australia. Mwezi Julai Gauff, mwenye miaka 15, aliingia kwenye jukwaa kubwa kwa kishindo baada ya kumshinda Williams, mwenye miaka 39 ambaye ni mshindi mara saba wa Grand Slam kwa mchezaji mmoja mmoja katika uwanja wa Wimbledon. Naye Muingereza Johanna Konta, atacheza na Mtunisia Ons Jabeur. Kwenye droo ya wanaume Muingereza Dan Evans atakutana na Mmarekani Mackenzie McDonald huko Melbourne. Evans, mwenye miaka 29, anacheza kwa mara ya kwanza kwenye Slam kama mchezaji mwanaume anayeongoza na anaweza kupambana na bingwa mtetezi Mserbia Novak Djokovic katika raundi ya tatu. Hata hivyo Djokovic, anayelenga kuongeza taji la nane hataanza kwa wepesi baada ya kupangiwa kucheza na Mjerumani ambaye ni namba 37 duniani Jan-Lennard Struff. Michuano ya kwanza ya Grand Slam ya mwaka huu inaanza Jumatatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako