• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China awataka watu wa Yemen kuendelea na njia ya utatuzi wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2020-01-17 10:04:14

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amezitaka pande mbalimbali nchini Yemen kuendelea kufuata njia ya utatuzi wa kisiasa.

    Bw. Wu amesema pande mbalimbali nchini Yemen zinatakiwa kufanya juhudi katika utekelezaji wa makubaliano ya Stockholm na makubaliano ya Riyadh na kuanzisha mapema mchakato wa pande zote unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.

    Bw. Wu amesema ingawa utekelezaji wa makubaliano ya Stockholm umekwama, makubaliano hayo yaliyosainiwa kati ya serikali na kundi la waasi la Houthi yametoa mchango katika kupunguza hali ya wasiwasi ya mkoa wa Hodeidah na kuhimiza mazungumzo kati ya pande mbalimbali za Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako