• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 11 wa Marekani wajeruhiwa katika shambulizi la makombora kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Iraq

    (GMT+08:00) 2020-01-17 15:54:37

    Askari 11 wa jeshi la Marekani wamejeruhiwa katika shambulizi la makombora lililofanywa wiki iliyopita katika kambi ya jeshi la Marekani nchini Iraq.

    Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Kamandi Kuu ya Marekani Kapteni Bill Urban imesema, wakati hakuna askari wa Marekani aliyeuawa katika shambulizi lililofanywa Januari 8 na Iran katika kambi ya jeshi la anga ya Al Asad, askari kadhaa wamepewa matibabu kutokana na dalili za kupata mshtuko kutokana na shambulizi hilo.

    Taarifa hiyo imesema, baadhi ya askari wamefanyiwa vipimo baada ya shambulizi hilo ikiwa ni hatua ya tahadhari, na dalili hizo ziligundulika.

    Zaidi ya askari 5000 wa Marekani wako nchini Iraq kulisaidia jeshi la nchi hiyo kupambana na wapiganaji wa kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako