• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema itashirikiana na nchi zinazohusika katika ajali ya ndege ya Ukraine

    (GMT+08:00) 2020-01-17 18:27:35

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Abbas Mousavi amesema, nchi hiyo imetoa ushirikiano na nchi ambazo raia wake walikuwa katika ndege namba PS-752 ya Ukraine iliyoanguka pembezoni mwa mji mkuu wa Iran, Tehran, mapema mwezi huu.

    Mousavi amesema watu wote waliofariki kwenye ajali hiyo wametambuliwa na uchunguzi wa kitaalam na ushirikiano vinaendelea vikijumuisha pande zote zinazohusika.

    Abiria wote 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya Ukraine waliuawa baada ya kupigwa na kombora lililorushwa kutoka ardhini na Iran Januari 8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako