• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia kutunga sheria mpya dhidi ya ukatili wa kijinsia

    (GMT+08:00) 2020-01-17 19:44:51

    Wizara ya sheria ya Namibia jana imesema serikali ya nchi hiyo inatunga sheria mpya ili kukabiliana na ongezeko la ukatili wa kijinsia.

    Wizara hiyo imesema, sheria hiyo itatoa nafasi kwa kifungo cha muda mrefu jela, na kuongeza kuwa kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zinatokana na mambo kadhaa ikiwemo ukosefu wa ajira au kunywa pombe kwa kupita kiasi.

    Polisi nchini Namibia imesema, idadi ya kesi za ukatili wa kijinsia zilizorekodiwa mwaka jana ilifikia zaidi ya elfu saba, na kesi 2,600 kati ya hizo zilifutwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako