• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yakanusha kukabiliwa na shinikizo la kuacha matakwa yake kwenye mazungumzo kuhusu bwala la mto Nile

    (GMT+08:00) 2020-01-18 18:04:23

    Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya Misri imekanusha kuwa ilikabiliwa na "shinikizo lolote la kuacha baadhi ya matakwa yake" kwenye mazungumzo kuhusu Bwawa Kubwa la Ethiopia GERD mjini Washington.

    Mawaziri wa mambo ya nje na maofisa wa rasilimali maji kutoka Misri, Ethiopia na Sudan walifikia makubaliano ya awali Jumatano baada ya siku tatu za mikutano mjini Washington na waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na rais wa Benki ya Dunia David Malpass. Nchi hizo tatu zilikubaliana kukutana mjini Washington tarehe 28 na 29, Januari ili kufikia makubaliano ya mwisho kuhusu kujazwa na kuendeshwa kwa bwawa hilo.

    Bwawa hilo ambalo limejengwa tangu mwaka 2011 kwenye mto Blue Nile katika nyanda za juu kaskazini mwa Ethiopia unatarajiwa kuzalisha umeme wa megawati elfu sita na kuwa bwawa kubwa zaidi la kuzalisha umeme barani Afrika. Hata hivyo, maofisa wa Misri wana wasiwasi kuwa kujaza bwawa hilo kwa haraka sana kunaweza kupunguza maji ya mto Nile yanayofikia Misri. Ethiopia inataka kujaza bwawa kwa mita za ujazo bilioni 74 katika miaka mitano hadi sita ijayo, huku Misri ikitaka kuongeza muda huo ili kuepuka matokeo mabaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako