• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia na China zina msimamo mmoja katika masuala makubwa ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-01-18 19:23:27

    Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov amesema Russia na China zina msimamo mmoja katika masuala makuu ya kimataifa

    Akiongea na wanahabari jana huko Moscow kwenye mkutano wa mwaka wa kufanya hitimisho kuhusu matokeo ya shughuli za kidiplomasia za Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia katika mwaka jana, Bw. Lavrov alisema uhusiano wa wenzi wa uratibu wa kimkakati wa pande zote kati ya Russia na China umeimarishwa zaidi katika mwaka 2019, jambo ambalo

    ni muhimu sana katika kutuliza mazingira ya sasa ya kimataifa.

    Bw. Lavrov ameongeza kuwa, msimamo wa Russia na China kuhusu amani na maendeleo ya dunia umebainishwa kwenye nyaraka nyingi zilizosainiwa na marais wa nchi hizo mbili, ambazo zimeinua uhusiano wa nchi hizo mbili kwenye ngazi mpya. Amesisitiza kuwa Russia na China zimekuwa zikifanya uratibu na kuungana mkono chini ya mfumo wa Umoja wa Mataifa na kushikilia kanuni ya msingi inayotetewa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako