• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZTE na MTN zafanya majaribio ya 5G

    (GMT+08:00) 2020-01-19 15:25:23

    Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China ZTE na kampuni ya huduma za mawasiliano ya Uganda MTN zimefanya hafla ya kuanzishwa kwa majaribio ya matumizi ya teknolojia mawasiliano ya 5G mjini Kampala Uganda. Upimaji wa kasi ya mtandao wa 5G na roboti zimeoneshwa kwenye hafla hiyo.

    Waziri mkuu wa Uganda Bw. Ruhakana Rugunda, mkurugenzi mtendaji wa kamati ya mawasiliano ya simu ya Uganda Bw. Godfrey Mutabazi, mkurugenzi mtendaji mkuu wa MTN Bw. Wim Vanhelleputte, na naibu mkurugenzi wa tawi la Afrika ya Kusini la ZTE Bw. Yi Yahua wamehudhuria hafla hiyo.

    Bw. Rugunda amesema serikali ya Uganda inaunga mkono maendeleo ya teknolojia, ili kutatua matatizo na changamoto ya maisha ya watu. Ana matarajio makubwa kuhusu mchango wa teknolojia ya 5G kwa maendeleo ya uchumi wa Uganda.

    Bw. Mutabazi amesema Uganda itakuwa nchi ya kwanza itakayotumia teknolojia ya 5G katika Afrika ya Mashariki, na kuwa nchi ya tatu yenye teknolojia hiyo barani Afrika baada ya Afrika Kusini na Nigeria. Bw. Vanhelleputte amesema MTN itahimiza matumizi ya kibiashara ya 5G nchini Uganda katika miaka miwili hadi mitatu ijayo, ili kuwapatia wateja huduma nzuri zaidi za matibabu, elimu na fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako