• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya kusimamia kukomesha uhasama nchini Sudan yafanya mkutano wa kwanza

    (GMT+08:00) 2020-01-19 17:27:46

    Baraza la mamlaka la Sudan limetoa taarifa kuwa kamati ya pande tatu ya kusimamia kukomesha uhasama kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile limefanya mkutano wake wa kwanza huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

    Mkutano huo umewakutanisha maofisa kutoka Sudan Kusini kama wapatanishi, na wawakilishi wa serikali ya Sudan na kundi la waasi la harakati ya ukombozi wa watu wa Sudan, tawi la Kaskazini SPLM-N.

    Kamati hiyo ilikagua hali ya kibinadamu katika majimbo hayo mawili na mipango inayohusiana na kazi ya kamati. Kamati hiyo itahamia Khartoum na kuunda makao makuu mjini Kadugli, Kordofan Kusini na mjini Damazin, Blue Nile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako