• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa usalama wa Kenya wazuia jaribi la shambulizi la Al-Shabaab Lamu

    (GMT+08:00) 2020-01-19 20:55:47

    Idara za usalama za Kenya zimevunja jaribio kubwa la shambulizi la kigaidi la kundi la al-Shabaab lililowalenga wanakijiji katika kaunti ya Lamu usiku wa jumamosi.

    Mkuu wa Kaunti ya Lamu Bw Irungu macharia amesema wapiganaji wa kundi hilo waliokuwa wamesheheni silaha walivamia kijiji cha Pandaguo na kulikuwa na mapambano ya muda wa saa saba, kabla ya magaidi hao kushindwa na kukimbilia kwenye msitu wa Boni.

    Amesema magaidi hao walianza shambulizi lao saa nne na nusu usiku ambalo liliendelea hadi saa tisa na nusu usiku wa kuamkia jumapili kabla ya kutimulia.

    Wanakijiji wameripoti kuwa wapiganaji takribani 50 walijaribu kuingia kwenye kijiji chao, lakini milio ya bunduki kutoka kwenye kituo cha polisi kijijini hapo iliwazuia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako