• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatangaza kupambana na waingizaji wa vifaa haramu vya uvuvi

    (GMT+08:00) 2020-01-20 08:58:52

    Mamlaka nchini Tanzania imetangaza kuanzisha kampeni maalum ya kupambana na vifaa haramu vya uvuvi na kusema matumizi ya vifaa hivyo yanaathiri sekta ya uvuvi nchini Tanzania.

    Waziri wa mifugo na uvuvi wa Tanzania Bw. Luhanga Mpina amesema serikali itaimarisha ukaguzi na udhibiti kwenye forodha zote kuhakikisha kuwa hakuna vifaa haramu vya uvuvi vinavyoingia Tanzania. Akiongea mjini Dar es salaam kwenye ziara ya kiwanda cha nyavu cha Nyotaventure, amesema waagizaji wa vifaa vya uvuvi wanaoingiza vifaa vibaya watachukuliwa hatua kali.

    Bw. Mpina amesema vifaa vya uvuvi vinavyotengenezwa nchini Tanzania vina ubora wa juu, na kuwataka watengenezaji wa Tanzania kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako