• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washiriki wa mkutano wa Berlin wakubali kuheshimu vikwazo vya silaha nchini Libya

    (GMT+08:00) 2020-01-20 09:02:22

    Washiriki wa mkutano kuhusu suala la Libya ulioitishwa na Ujerumani wamekubali kuheshimu vikwazo vya silaha na usitishaji vita nchini Libya, huku wakiahidi kuanzisha utaratibu wa usimamizi ili kuhakikisha amani ya kudumu.

    Baada ya mkutano huo Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amewaambia wanahabari kuwa mkutano huo umetoa mchango muhimu katika kusukuma mbele juhudi za kuleta amani nchini Libya, washiriki wote wamekubali kuwa suala la Libya linahitaji utatuzi wa kisiasa, na kamwe halitatatuliwa kwa uingiliaji wa kijeshi. Ameongeza kuwa suala hilo haliwezi kutatuliwa ndani ya siku moja, lakini mkutano huo ni hatua ya kwanza na umeweka mwelekeo sahihi kwa hatua zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako