• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Blak Blad yajiondoa eneo hatari kwa kuilipua Western Bulls 44-0 kwenye Ligi Kuu ya raga Kenya

    (GMT+08:00) 2020-01-20 09:19:06

    Wenyeji Blak Blad walifufua matumaini ya kukwepa kuangukiwa na shoka baada ya kuilipua Western Bulls 44-0 kwenye Ligi Kuu ya raga (Kenya Cup) katika Chuo Kikuu cha Kenyatta jijini Nairobi. Mchezaji Arcadius Khwesa alikuwa shujaa wa Blak Blad akichangia miguso mitatu muhimu. Ushindi huu unatarajiwa kuiondoa Blak Blad katika mduara hatari wa kutemwa na wakati huohuo kusukuma Bulls kwenye maeneo hayo hatari. Bulls, ambayo imerejea katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kushushwa msimu 2016-2017, iliingia mchuano huo wa raundi ya 11 ikifunga mduara wa 10-bora kwa alama 13 katika ligi hii ya klabu 12 nayo Blak Blad ilishikilia nafasi ya 11 kwa alama nane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako