• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kinachoendelea kwenye Timu ya Yanga SC baada ya kufungwa mechi mbili chini ya kocha Eymael

    (GMT+08:00) 2020-01-20 09:23:41

    Mlinzi wa klabu ya Yanga, Ally Mtoni ameomba radhi kufuatia kitendo cha kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC katika kipindi cha pili na kupelekea kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi. Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, ulishuhudia Yanga ikipoteza kwa bao 1-0. Naye kocha wa klabu ya Yanga, Luc Eymael ameonesha kutofurahishwa na waamuzi wa mchezo huo wa Jumamosi. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Eymael amesema kitendo alichofanyiwa na mwamuzi wa kati cha kukataa kumpa mkono amekitafsiri kama ni ubaguzi dhidi yake. Kuhusiana na mchezo kiufundi, kocha Eymael amesema kuwa bahati haikuwa upande wao katika mchezo huo, kwani walicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kutosha lakini hazikuzaa matunda na mwisho wakafungwa bao ambalo amesema hakuelewa limetokeaje. Kocha huyo sasa amepoteza mechi ya pili mfululizo katika ligi, akifungwa jumla ya magoli manne, huku timu yake ikiwa haijafunga bao lolote. Sasa mashabiki wengi wa Yanga wamefunguka wakiutaka uongozi wa timu hiyo uachane na kocha mpya. Kutokana na mwendelezo wa matokeo hayo, wengi wao wamesema ni vema kazi hiyo akaendelea nayo Mkwasa sababu alianza kuirudisha timu katika morali tofauti na Luc ambaye amekuja kuanza upya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako