• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandamano dhidi ya serikali ya Iraq yapamba moto kutokana na kasi ndogo ya utekelezaji wa mageuzi

    (GMT+08:00) 2020-01-20 09:54:11

    Mamia ya vijana wa Iraq jana wamechochea zaidi upinzani dhidi ya serikali ya Iraq kutokana na kasi ndogo ya mchakato wa mageuzi ya kisiasa ya serikali.

    Ofisa wa wizara ya mambo ya ndani ya Iraq amesema mamia ya waandamanaji jana walikusanyika kwenye uwanja wa Tayran na uwanja wa Wathba karibu na uwanja wa al-Tahrir, ambapo walipambana na polisi huku wakichoma moto makumi ya magurudumu, na kuzuia barabara kuu iitwayo Mohammed al-Qassim inayounganisha mji mkuu wa Baghdad na jamii zilizoko mashariki mwa mji huo.

    Ameongeza kuwa polisi walirusha mabomu ya machozi na kufyatua risasi angani ili kuwatawanya waandamanaji, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine takriban 30 kujeruhiwa na kubanwa pumzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako