• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wafanya maandalizi ya sherehe za mwaka mpya

    (GMT+08:00) 2020-01-20 10:07:20

    Raia wa China nchini Kenya pamoja na baadhi ya wakenya jana waliungana pamoja kwa sherehe za makabirisho ya mwaka mpya wa jadi wa China.

    Sherehe hizo zilifanyika katika jumba la China Centre jijini Nairobi.

    Mamia ya watumbuizaji walipanda jukwaani katika sherehe za kuukaribisha mwaka jadi wa jadi wa China zilizofanyika katika jumba la China Centre jijini Nairobi kushiria kuanzisha mwaka mpya wa jadi China ambapo mwaka huu ni mwaka wa Panya.

    Michezo ya kijadi, burudani za hapa na pale pamoja na shughuli nyingine za kiburudani ni baadhi ya mambo yaliyopambwa wakati wa tukio hilo.

    Guo Wei,mchina nayeishi Kenya anaelezea umuhimu wa sikukuu hii ya mwaka mpya kwa wachina.

    "Tungependa kuonyesha furaha yetu ya mwaka mpya wa jadi wa China maarufu kama spring festival pamoja na marafiki zetu wakenya.Na wakati wa sikukuu ya spring watu wataeleza hisia zao,matarajio yao ya siku za baadae,kutumiana salamu za heri na pia kueleza matarajio yao ya mwaka mpya"

    Sikukuu ya Spring ni Mwaka Mpya wa jadi wa China, ni sikukuu ya jadi na muhimu kabisa nchini China. Wachina wameshasherehekea sikukuu hii kwa zaidi ya miaka 4000 sasa. Emmanuel ni mkenya aliyealikwa na kushirikia katika sherehe hizi hapa China Centre jijini Nairobi.

    Chris naye pia hakuachwa nyuma,anasema inapofika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China hupata fursa ya kuonja vyakula vitamu vya kichina.

    Wakati wa sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina, idara za utamaduni hushirikisha michezo ya sanaa ya aina mbalimbali. Kwa mfano, usiku wa mkesha vituo vya televisheni huonyesha sherehe maalumu ya michezo toka saa mbili za usiku hadi saa saba usiku, ambapo huwepo watazamaji zaidi ya milioni mia moja.

    Kila mwaka taifa la China huwa na utamaduni wa kusherehekea mwaka wake mpya wa kichina na mwaka huu imeangukia Januari 25 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako