• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENNIS: Federer aingia raundi ya pili ya mashindano ya Australian Open

    (GMT+08:00) 2020-01-20 18:17:56

    Roger Federer amemshinda Steve Johnson na kufanikiwa kuingia katika raundi ya pili ya mashindano ya tennis ya Australian Open katika juhudi zake za kusaka taji la 21 la Grand Slam. Kabla ya pambano hilo, Federer mwenye umri wa miaka 38, alisema hana matarajio makubwa na pambano hilo baada ya kukosa mazoezi ya awali kwa kuwa alitaka kuwa na muda mrefu na familia yake. Amefurahia ushindi huo na kusema alifanya vizuri mazoezi na imedhihirika katika ushindi alioupata dhidi ya Steve Johnson. Wakati Federer akifurahia ushindi huo, hali ni tofauti kwa aliyekuwa mchezaji namba moja wa tennis kwa wanawake Venus Williams ambaye ameshindwa kwa mara ya pili na Coco Gauff kwenye mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako