• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiti kirefu cha mbao chaanguka na kusababisha watu zaidi ya mia moja kujeruhiwa kwenye mkusanyiko wa kidini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:07:15

    Kiti kirefu cha mbao kilianguka ghafla na kusababisha watu zaidi ya mia moja kujeruhiwa, wakati maelfu ya wakristo wa madhehebu ya Orthodox wakijumuika kwenye mji wa Gondar, kaskazini magharibi mwa Ethiopia, ili kusherehekea sikukuu ya Epifania.

    Shirika la habari la AMMA limemnukuu mkuu wa idara ya amani na usalama ya mji wa Gondar Bw. Tesfa Mekonen akisema, tukio hilo limetokea wakati kiti kirefu kilichotengenezwa kutoa mahali pa kukaa kikianguka kutokana na kubeba uzito unaozidi uwezo wake.

    Lakini ofisa huyo hakutaja idadi ya vifo vilivyotokana na tukio hilo.

    Kwa mujibu wa Bw. Mekonen, wawili kati ya majeruhi ni raia wa kigeni, lakini idara hiyo haikutaja uraia wa wageni hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako