• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Tanzania lasifu mageuzi ya serikali kwenye sekta ya madini

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:11:46

    Kamati ya kudumu ya nishati na madini katika Bunge la Tanzania imesifu mageuzi makubwa ya serikali kwenye sekta ya madini.

    Kamati hiyo imesema mageuzi kwenye sekta ya madini yaliyoanzishwa na rais John Magufuli yameanza kuinufaisha Tanzania, ikiwa ni pamoja na ongezoko la mapato ya kodi kwenye sekta hiyo na manufaa mengine.

    Wizara ya madini ya Tanzania imewasilisha ripoti ya utekelezaji ya nusu mwaka wa fedha wa 2019/2020 mjini Dodoma, ambayo imeonyesha kuwa mapato ya kodi kwenye sekta ya madini yamefikia dola takriban milioni 105 za kimarekani hadi tarehe 31 mwezi Desemba mwaka jana. Na idadi ya jumla ya uuzaji wa dhahabu imefikia kilogram 5,546 kuanzia mwezi Julai hadi Novemba mwaka jana huko Geita, Chunya, Kahama, Mwanza na Mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako