• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Coco Gauff amshinda tena Venus Williams na kusonga mbele raundi ya pili

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:31:32

    Kinda mwenye miaka 15 Coco Gauff amethibitisha kuwa ushindi alioupata mwaka jana dhidi ya Venus Williams haukuwa fluku dudu baada ya kumshinda tena bingwa mara saba wa Grand Slam na kuingia raundi ya pili ya michuano ya wazi ya Australia. Gauff alitangaza ujio wake kwenye mchezo wa tenisi Julai mwaka jana alipovaana na Williams, mwenye miaka 39, kwenye raundi ya kwanza ya michuano ya Wimbledon. Na kama mara iliyopita, amefanikiwa kumshinda kwa seti 7-6 (7-5) 6-3. Mechi inayofuata Gauff atacheza na Mromania namba 74 duniani Sorana Cirstea. Gauff, aliyeingia Wimbledon baada ya mechi za kufuzu na baadaye kupewa mwaliko wa kucheza kwenye droo ya michuano ya wazi ya Marekani mwezi Septemba, ameingia kwa mara ya kwanza kwenye droo kuu ya Grand Slam kama mchezaji aliyefuzu moja kwa moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako