• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa Harambee Starlets Vivian Corazon kusainiwa kwenye klabu ya Atletico Madrid

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:37:11

    Kiungo wa timu ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets Vivian Corazon Odhiambo amesema kujiunga na klabu kubwa ya Hispania kwa upande wa wanawake Atletico Madrid ni ndoto yake iliyotimia. Odhiambo anaondoka nchini Kenya Jumatano na anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja. Katika msimu uliopita wa ligi ya divisheni ya kwanza yenye timu 16, klabu ya Atletico Madrid ilimaliza ya pili ikiwa na pointi 36, pointi 10 nyuma ya mabingwa Barcelona. Odhiambo mwenye miaka 21 ameichezea klabu ya Gaspo FC, iliyomaliza ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Wanawake. Alikuwa akiwindwa wakati Kenya ilipocheza mechi ya kufuzu Olimpiki dhidi ya Ghana. Mwaka uliopita timu ilishinda 1-0 kwa wingi wa magoli na kusonga mbele raundi ya nne ambako walibanjuliwa na Zambia kwa 2-1. Pia alikuwa mmoja wa wachezaji wa timu ya Starlets iliyoshinda michuano ya kombe la Chalenji la wanawake baada ya kuwagaeagaza mabingwa Tanzania 2-0 kwenye mechi ya fainali iliypigwa uwaja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako