• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aston Villa yatangaza rasmi kumsajili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta

    (GMT+08:00) 2020-01-21 10:37:35

    Klabu ya Aston Villa imetangaza rasmi kumsajili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta akitokea KRC Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne na nusu. Samatta atakuwa Villa Park hadi 2024. Kocha wa Aston Villa Dean Smith akiongea na wanahabari mapema jana alisisitiza kuwa mchezaji huyo kila kitu kimekamilika bado vitu vidogo tu. Hata hivyo Samatta mwenye miaka 27, hataweza kucheza mchezo wa leo wa Aston Villa dhidi ya Watford kwa kuwa hakupata muda wa kutosha kuwa na timu hiyo kutokana na kuchelewa kupata kibali cha kazi. Dean Smith anasema kuwa hataweza kumtumia Samatta katika mchezo wa leo dhidi ya Watford kwa sababu ya kuchelewa kwa jina lake kuwa kwenye list ya wachezaji watakaocheza katika uwanja wa Villa Park dhidi ya Watford, pamoja na hayo Dean Smith amesema anahitaji mshambuliaji mwingine tena aongezwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako