• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zasaini makubaliano ya kusawazisha sera za uhamiaji

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:12:07

    Mawaziri wa leba kutoka nchi za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika wamesaini makubaliano ya kusawazisha sera zao za uhamiaji.

    Mawaziri hao waliokutana mjini Nairobi, Kenya kwenye mkutano wa kikanda kuhusu uhamiaji wa nguvukazi ndani na nje ya kanda, wamesema makubaliano hayo yatasimamia na kuhimiza uhamiaji wa nguvukazi ulio salama na ulioratibiwa, kuendana na vigezo vya kimataifa na kikanda.

    Kwenye mkutano na wanahabari baada ya mkutano huo, Waziri wa leba wa Kenya Simon Chelugui amesema wamekubaliana kutekeleza mipango ya kikanda na kibara, kuhusu uhuru wa kusafiri ili kuhimiza fursa za ajira, kuzuia uhamiaji usio wa kawaida, na kupambana na magendo na ajira za kulazimishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako