• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa Panda Pack wa China waendelea kuleta tabasamu kwa watoto maskini Namibia

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:12:27

    Watoto 1,075 kutoka Mradi wa Monte Christo, wanaoishi katika eneo la makazi duni la Havana katika mji mkuu wa Namibia Windhoek, watanufaika na Mradi wa Panda Pack kufuatia hafla ya kukabidhi mabegi ya shule iliyofanyika jana Jumanne.

    Mabegi ya shule yalikabidhiwa kwa shule hiyo na Ubalozi wa China nchini Namibia kwa kushirikiana na Mfuko wa China wa Kupunguza Umaskini CFPA.

    Balozi wa China nchini Namibia Bw. Zhang Yiming amesema mradi huo unalenga kuwasaidia watoto wa Namibia kupata elimu bora. Mradi wa Panda Pack ulioanzishwa na CFPA na Mfuko wa One Economy wa Namibia chini ya uungaji mkono wa Wizara ya elimu ya Namibia, ulichangia mabegi elfu 10 ya shule mwaka 2018, na mwaka jana zaidi ya mabegi elfu 40 yalitolewa kwa watoto katika mikoa 15 nchini Namibia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako