• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania awahakikishia wanadiplomasia kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 utakuwa wa amani

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:18:16

    Rais John Magufuli wa Tanzania amewahakikishia wanadiplomasia walioko Tanzania kuwa Tanzania itakuwa na uchaguzi wa amani, huru na haki utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

    Akiongea na wanadiplomasia kwenye tafrija ya mwaka mpya Ikulu mjini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema waangalizi wa kimataifa watakaribishwa kushuhudia jinsi demokrasia ya Tanzania inavyozidi kupevuka.

    Zaidi ya watanzania milioni 20 kati ya watanzania milioni 55 wanatarajiwa kupiga kura kwenye uchaguzi huo, kumchagua rais, wabunge na madiwani. Rais Magufuli amewashukuru mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa walioko Tanzania, kwa kuunga mkono mageuzi yanayoongozwa na serikali yake, yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye mapato ya kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako