• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya wanariadha 3,000 kushiriki mbio za Eldoret

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:46:36

    Wanariadha nyota wanatarajiwa kushiriki kwenye mbio kubwa za mabingwa za nyika zinazofanyika kila mwaka katika klabu ya Eldoret Sports, kaunti ya UasinGishu siku ya Jumapili. Mbio za mwaka huu zikiwa za 29, zimevutia zaidi ya wanariadha 3,000 miongoni mwao ni mshika rikodi wa mbio za nusu marathoni duniani Geoffrey Kamworor, bingwa wa mita 5,000 chini ya miaka 20 Beatrice Chebet, bingwa aliyepata medali ya dhahabu kwa mbio za mita 5,000 chini ya miaka 20 Edward Zakayo, mshindi wa nusu marathoni ya Family Bank Nancy Jelagat na wengine wengi. Naye mshika rikodi wa nusu marathoni duniani Brilliant Jepkorir, ambaye alikuwa wa pili wikiendi iliyopita kwenye mbio za nusu marathoni za Houston atafanya kampeni ya kutetea taji lake la km 8 kwenye mbio za wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako