• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United yashtakiwa na FA kwa mwenendo mbaya wa mchezaji

    (GMT+08:00) 2020-01-22 09:47:13

    Manchester United inashtakiwa na Shirikisho la Soka la Uingereza kwa kwa kushindwa kuhakikisha kuwa wachezaji wake wanafuata utaratibu katika mechi waliyoshindwa 2-0 na Liverpool Jumapili. Mashtaka hayo yanahusiana na tukio ambapo wachezaji wa United walimkabili mwamuzi Craig Pawson baada ya awali kuruhusu goli lililofungwa na mchezaji wa Liverpool Roberto Firmino. Hata hivyo msaidizi wa refa VAR iliamua sio goli, baada ya faulu ya Virgil van Dijk kwa mlinda mlango David de Gea. United wana hadi Alhamis kujibu. Tukio hilo, lilitokea dakika 26 wakati Liverpool inaongoza bao1-0, na kushuhudiwa De Gea akimshambulia Pawson.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako