• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ngassa afungiwa, kocha wa Yanga aonywa

  (GMT+08:00) 2020-01-23 18:39:01

  Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara imewakuta na hatia wachezaji watatu wa Yanga, Mrisho Ngassa, Ramadhani Kabwili, na Cleofas Sospeter, hivyo kuwafungia kucheza michezo mitatu pamoja na faini ya laki 5 kila mmoja. Kamati hiyo iliyokutana Jumatatu wiki hii, pia ilitoa onyo kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Luc Eymael kwa kutoa matamshi yasiyofaa kuhusu ubaguzi wa rangi dhidi yake. Eymael alitoa kauli hiyo wakati Yanga ikifunga bao 1 – 0 dhidi ya Azam FC katika mechi iliyochezwa Januari 18 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako