• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vita vya kibiashara vyaiponza Uganda dola milioni 454.

    (GMT+08:00) 2020-01-28 19:02:55
    Mzozo wa kibiashara mipakani kati ya Uganda na mataifa jirani imeaathri sana ukuaji wa biashara nchini humo.

    Kulingana na ripoti za Benki kuu ya Uganda, Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru na ile ya maendeleo ya zao la kahawa nchini humo, taifa la Uganda limepoteza dola milioni 454.7 kufikia mwezi Desemba mwaka uliopita, kwa bidhaa ambazo huuzwa nje.

    Kulingana na ripoti hiyo, Uganda ilipoteza pesa nyingi kutoka kwa taifa la kenya na Rwanda ikilinganishwa na mataifa mengine ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Uuzaji wa bidhaa kwa taifa la Rwanda, ulipungua hadi dola milioni 173 mwaka wa 2019, kutoka dola milioni 925 mwaka wa 2018.

    Uuzaji wa bidhaa za Uganda nchini Kenya ulipungua hadi dola milioni 535 mwaka wa 2019, kutoka dola milioni 825 mwaka wa 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako