• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kutumia kilimo kutatua ukosefu wa ajira kwa vijana.

    (GMT+08:00) 2020-01-28 19:08:48
    Serikali ya Tanzania imeamu kutumia sekta ya kilimo kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana. Kwa muda mrefu, kilimo kimekuwa kikichukuliwa kama kazi ya ziada baada ya kukosa ajira maeneo mengine. Haya ni kwa mujibu wa naibu waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana na ajira, Anthony Mavunde.

    Waziri Mavunde anasema kwamba wizara yake inajitolea katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo, ambapo mpango wa serikali kwa sasa ni kuhakikisha asilimia 40 ya watu milioni 24.3 wanaajiriwa kwenye sekta ya kilimo.

    Aidha anasisitiza kwamba malengo ya serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka wa 2025, asilimia 40 ya nguvu kazi ya nchi inaajiriwa kwenye sekta ya viwanda ambayo ni mnyororo wa thamani na ambayo imekuwa ikianzia kwenye mazao ya kilimo,ufugaji na misistu na huko mahitaji ya malighafi zitokanazo na mazao ya kilimo zitakuwa ni kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako