• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenyatta afungua kiwanda cha saruji

    (GMT+08:00) 2020-01-29 19:51:44
    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefungua kiwanda cha kutengeneza saruji chenye thamani ya Sh5.8 eneo la Salgaa, Kaunti ya Nakuru ambacho kinatarajiwa kuchangia upatikanaji wa ajira nchini Kenya.

    Kiwanda hicho cha Simba Cement kina uwezo wa kutoa nafasi 700 za ajira na kitastawisha sekta ya ujenzi wa nyumba kwa kuwezesha upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu.

    Kiwanda hicho ambacho kingali kinapanuliwa tayari kimewaajiri Wakenya 300 na inakisiwa kuwa kufikia mwezi Juni 2020 kitachangia kubuniwa kwa nafasi zaidi za ajira.

    Aidha rais amezihimiza kampuni zinazohusika na sekta ya ujenzi kutumia saruji ya gharama nafuu kutoka kiwanda hicho kupanua biashara zao na akatoa hakikisho kuwa serikali inamakinika kuvutia viwanda zaidi katika eneo hilo.

    Kwa upande wake waziri wa Mafuta na Uchimbaji Madini John Munyes amesema hitaji la saruji sasa limeongezeka nchini Kenya na katika kanda ya Afrika mashariki ikiwemo Sudan Kusini na Kusini mwa Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako