Maleko alisema kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwazuia wanawake wengi kufanya biashara hizo, ukizingatia Tanzania imepata fursa ya uwapo wa soko la pamoja la Afrika Mashariki, lakini bado wanawake wengi hawajalitumia.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo, chama hicho kiliandaa mkakati wa kuhakikisha kinazunguka nchi nzima na kukutana na wanawake wajasiriamali ili kuwapatia elimu ya ufanyaji biashara hiyo ambapo wamepanga hadi kufikia mwaka 2023 kuwafikia wanawake 10,000.
Alisema mbali na kuwapatia elimu na mbinu za kufanya biashara hizo, chama hicho kimekuwa kikitumia fursa hiyo kuwapatia mikopo yenye riba nafuu kama mitaji pamoja na kuwaelimisha juu ya kutunza kumbukumbu za kifedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |