• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kuandaa awamu ya pili ya Siku ya Kahawa ya Kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-01-31 09:53:40

    Ethiopia inapanga kuandaa awamu ya pili ya Siku ya Kahawa ya Kimataifa, tarehe 6 mwezi ujao mjini Addis Ababa, ambayo yatahudhuriwa na watu 1,500 wakiwemo maofisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia, wajumbe wa kampuni ya kahawa na wataalam.

    Mkurugenzi wa uhusiano wa umma na mawasiliano wa idara ya kahawa na chai ya Ethiopia Bw. Sahlemariam Gebremedhin amesema, shughuli hiyo ni jukwaa zuri la kuitangaza kahawa ya Ethiopia kwa dunia nzima.

    Habari zinasema maonyesho hayo ya siku tatu yenye kauli mbiu ya "kahawa kutoka ardhi ya asili" yatajumuisha mikutano, maonyesho, sherehe na shughuli nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako