• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadao wa mazao ya misitu watakiwa kuzingatia ubora

    (GMT+08:00) 2020-01-31 19:41:29
    Serikali imeutaka Umoja wa wenye Viwanda vya Mazao ya Misitu Kanda ya Kaskazini (NOFIA), kuzingatia ubora wa uchakataji wa mazao hayo ili kushindana katika masoko ya nje.

    Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, alipokuwa akifungua Mkutano wa 10 wa Wanaviwanda Wadogo na wa Kati wanaochakata mazao yatokanayo na misitu katika kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara.

    Prof. Silayo alisema ni vyema wanachama hao wakazalisha kwa ubora ili wapate masoko nje ya nchi, na kwamba tayari serikali imeshafanya mawasilianao na Kenya na Zambia ambao wamekubali kutuma wataalamu wao kuja kutembelea mashamba hayo kwa lengo la kuingia makubaliano katika uwekezaji na kuweka mkataba wa biashara hiyo.

    Prof. Silayo aliwataka wadau hao kuhakikisha kila mmoja anatoa bidhaa zenye ubora na kuwekeza kwenye teknolojia mpya kukabiliana na ushindani kwenye soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako