• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wa Makerere waunda mtambo wa kufuatilia ubora wa hewa

    (GMT+08:00) 2020-01-31 19:42:21
    Kundi la wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wametengeneza mashine zinazofuatilia ubora wa hewa na kuweka mitambo mjini Kampala na maeneo mengine ya nchi.

    Kiongozi wa mradi huo wa AirQo Bwana Mhandisi Bainomugisha, , alisema teknolojia hiyo inakusanya na kutoa data muhimu kuhusu hewa.

    Kulingana na Bwana Bainomugisha, data zao kuhusu utoaji wa gesi chafu na ubora wa hewa zinatoa ushahidi kuhusu maamuzi ya serikali ya kuzuia uingizaji wa magari yaliyotumiwa zaidi ya miaka 15.

    Bwana Paul Green ambaye ni mshiriki wa kundi hilo, alisema data sahihi ni muhimu katika kuunda maamuzi na sera za kushughulikia maswala ya afya ya umma.

    Mtambo una sensa mbili za hewa, kifaa cha kuchunguza joto na unyevu na GPS ya kuonyesha eneo lake.

    Unaendeshwa kwa kutumia betri au nishati ya jua na data hiyo hupitishwa kwa programu hadi kwenye kituo baada ya kila dakika mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako