Wito huo umetolewa jana na Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Consolata Gabone.
Alisema kwa sasa kuna mashirika mengi yanayotoa huduma za bima za kilimo katika mikoa ya nyanda za juu kusini na kuwa ni wakati mwafaka kwa wakulima hao kujiunga na Bima za Kilimo kwajili ya manufaa yao.
Consolata alisema sekta ya kilimo imekuwa na mchango mkubwa sana kwajili ya maendeleo ya kilimo nchini na imekuwa ikichangia pato la taifa na hivyo ni muhimu kwa wakulima kujihakikishia usalama wa mazao yao kwa kukata bima za kilimo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |