• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuongeza vikwazo vya kusafiri kwa nchi nyingine sita

    (GMT+08:00) 2020-02-01 18:43:09

    Vyombo vya habari vya Marekani vimetangaza kuwa serikali ya Trump itaziwekea vikwazo nchi sita mpya kuingia nchini humo, hatua ambayo ina utata na imeshakuwa ikikosolewa.

    Vikiwanukuu maofisa kutoka idara ya Usalama wa Ndani na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, vyombo vya habari vikiwemo New York Times na gazeti la Wall Street vimesema Marekani itazuia raia kutoka Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar na Nigeria kuomba viza ambazo zitawafanya kuwa wakazi wa kudumu wa Marekani. Nchi nyingine mbili, Sudan na Tanzania, zitafungiwa kushiriki bahati nasibu ya kupata uraia wa kudumu wa Marekani 'Green Card.' Nchi hizo mpya zilizozuiwa zinasemekana kushindwa kufikia vigezo vya kutoa taarifa na usalama kwa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako