• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaadhimisha Siku ya taifa ya Mashujaa

    (GMT+08:00) 2020-02-02 18:39:12

    Rwanda imeadhimisha Siku ya taifa ya Mashujaa nchini kote kwa kutoa heshima kwa mashujaa wa kitaifa wa nchi hiyo.

    Rais Paul Kagame wa Rwanda, maafisa wakuu wa serikali na maafisa wa ubalozi jana walijiunga na familia za mashujaa waliokufa wa Rwanda kuweka mashada kwenye mnara wa mashujaa katika eneo la Remera, mjini Kigali.

    Aidha, Wanyarwanda wamekusanyika katika ngazi ya kijiji kuwakumbuka mashujaa hao.

    Waziri mkuu wa Rwanda Bw. Pierre Damien Habumuremyi amesema Rwanda nzuri na yenye mafanikio inatokana na kujitolea kwa mashujaa wa taifa, hivyo amewashukuru kwa ushujaa wao na kutoa wito kwa Wanyarwanda hasa vijana, wafuate nyayo za mashujaa na kufanya kazi kwa bidii kuhimiza moyo wao, ili kukuza umoja, uzalendo, ushirikiano na amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako