• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan apokea mwaliko wa kutembelea Marekani

    (GMT+08:00) 2020-02-03 08:40:50

    Mwenyekiti wa baraza la utawala nchini Sudan Bw. Abdel Fattah al-Burhan amepokea mwaliko rasmi kutembelea Marekani.

    Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema kwenye mazungumzo kwa njia ya simu, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Michael Pompeo amemwalika Bw. al-Burhan kutembelea Marekani ili wapitie makubaliano ya uhusiano kati ya nchi mbili na namna ya kuendeleza uhusiano wao. Bw. al-Burhan amekaribisha mwaliko huo na kuahidi kutekeleza hivi karibuni.

    Sudan ambayo imewekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani tangu mwaka 1997, na kuwa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi tangu mwaka 1993, imekuwa inafanya kazi ya kuishawishi Marekani iiondoe kwenye orodha hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako