• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa kutuma wanajeshi 600 zaidi kwenye eneo la Sahel

    (GMT+08:00) 2020-02-03 08:41:03

    Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Bibi Florence Parly amesema Ufaransa itatuma askari 600 zaidi kwenye eneo la Sahel ili kuimarisha operesheni zake za kijeshi kuwaondoa wapiganaji wa kiislamu.

    Taarifa iliyotolewa na Bibi Parly inasema wanajeshi hao watawekwa kati ya Mali, Burkina Faso na Niger, na wengine wanashirikishwa kwenye kikosi cha G5 cha Sahel. Bibi Parly amesema mapambano dhidi ya ugaidi ni jambo la kipaumbele katika eneo la Sahel, na Ufaransa iko mstari wa mbele lakini haiwezi kuwa peke yake.

    Hata hivyo hali ya usalama katika eneo la Sahel bado ni tete hasa kutokana na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa jihadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako