• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yatangaza dharura ya kitaifa kutokana na janga la nzige

    (GMT+08:00) 2020-02-03 08:53:06

    Somalia imetangaza kuingia kwenye hali ya dharura ya kitaifa kutokana na uvamizi wa nzige wa jangwani kwenye maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Wizara ya kilimo ya Somalia imesema, janga hilo inaweza kutishia usalama wa chakula nchini humo na kuathiri msimu mpya wa kilimo utakaoanza mwezi wa Aprili.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, ni muhimu kuchukua hatua kuwadhibiti nzige hao kwa haraka na kuwasaidia wakulima na wafugaji wanaoathiriwa.

    Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa mataifa FAO limesema tayari malisho na mazao yameathiriwa na nzige nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, na kuna hatari kubwa kwenye eneo hilo ambalo watu milioni 12 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, na wengi kati yao wanategemea zaidi kilimo kujikimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako