• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yazindua mjadala wa umma kuhusu rasimu ya katiba

    (GMT+08:00) 2020-02-03 08:58:05

    Somalia imezindua mjadala wa umma kuhusu rasimu ya katiba. Waziri wa mambo ya katiba wa nchi hiyo Bw. Salah Jama amesema wadau zaidi ya 100 wameshiriki kwenye mkutano wa kwanza wa wazi unaoendelea kwa siku tatu katika eneo la Benadir.

    Katika taarifa iliyotolewa na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Bw Jama anasema watu wa Somalia wanaoishi ndani na nje ya nchi wanaweza kushiriki kwenye majadiliano kwa njia mbalimbali zikiwemo mtandao wa internet, radio na televisheni, ili kukusanya maoni ya wasomali wote kuhusu masuala muhimu katika katiba ya muda, husuan masuala kama hadhi ya Mogadishu, namna ya kugawanya raslimali na madaraka, na jinsi ya kufanya uchaguzi.

    Kutokana na msaada wa jumuiya ya kimataifa, Somalia inafanya maandalizi ya uchaguzi mkuu, ambao utakuwa wa kwanza tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vitokee mwaka 1992. Mkurugenzi wa tume huru ya uchaguzi ya taifa Bw. Ismail Yasin Mohamed, amesema tume yake iko tayari kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako